Tanzania yataka kubadili TTCL kuwa shirika la Umma


Mwnyekiti wa bodi ya TTCL Mhandisi Omar Nundu akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya menejimenti ya TTCL na Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Ngonyani Makao makuu ya TTCL.

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  imesema inakusudia kutunga sheria  mpya ya  kampuni ya simu Tanzania TTCL  ili  kulifanya  kuwa shirika la umma  na iweze  kujiendesha kwa ufanisi.
Akizungumza na wadau mbalimbali katika mkutano wa kujadili mapungufu pamoja na mafaniko Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi  na Mawasiliano Bara Edwin Ngonyani amesema zoezi la kutunga sheria mpya limeanza ili kuliwezesha  shirika hilo  kufanya kazi kwa ufanisi na  kuendana na sera ya taifa ya Tehama  ya mwaka 2016 pamoja na sheria ya mitandao ya mwaka 2015 inayotaka kuwepo na miundombinu ya uhakika na salama.
Hata hivyo amesema  lengo kuu la kutungwa kwa sheria hiyo mpya ni kukuza uchumi na kuweza kuleta tija katika taifa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali za muda mrefu katika kampuni hiyo ambapo amesema  kuboreshwa kwake ni kutaka kuzalisha  kwa ufanisi.
Kwaupande wao baadhi ya wadau kutoka Zanzibar wametoa maoni juu ya ubadilishwaji huo wa sheria  kuzingatiwa  haki kwa pande zote mbili za muungano ili kuweka usawa katika ufanisi wa kazi  ili  kuepusha malalamiko  kati  ya bara na zanziabr.
 TTCL  ni mhimili mkuu katika kutoa huduma za mawasiliano  ya data katika ukanda  wa Afrika mashariki na kati,kusini mwa jangwa la sahara ambapo nchi hizo hutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano NICTBB.
Na:Amina Omar Zanzibar24

No comments