Tanzania yataka kubadili TTCL kuwa shirika la Umma
Mwnyekiti wa bodi ya TTCL Mhandisi Omar Nundu akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya menejimenti ya TTCL na Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Ngonyani Makao makuu ya TTCL. |
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesema inakusudia kutunga sheria mpya ya kampuni ya simu Tanzania TTCL ili kulifanya kuwa shirika la umma na iweze kujiendesha kwa ufanisi.
Akizungumza na wadau mbalimbali katika mkutano wa kujadili mapungufu pamoja na mafaniko Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Bara Edwin Ngonyani amesema zoezi la kutunga sheria mpya limeanza ili kuliwezesha shirika hilo kufanya kazi kwa ufanisi na kuendana na sera ya taifa ya Tehama ya mwaka 2016 pamoja na sheria ya mitandao ya mwaka 2015 inayotaka kuwepo na miundombinu ya uhakika na salama.
Hata hivyo amesema lengo kuu la kutungwa kwa sheria hiyo mpya ni kukuza uchumi na kuweza kuleta tija katika taifa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali za muda mrefu katika kampuni hiyo ambapo amesema kuboreshwa kwake ni kutaka kuzalisha kwa ufanisi.
Kwaupande wao baadhi ya wadau kutoka Zanzibar wametoa maoni juu ya ubadilishwaji huo wa sheria kuzingatiwa haki kwa pande zote mbili za muungano ili kuweka usawa katika ufanisi wa kazi ili kuepusha malalamiko kati ya bara na zanziabr.
TTCL ni mhimili mkuu katika kutoa huduma za mawasiliano ya data katika ukanda wa Afrika mashariki na kati,kusini mwa jangwa la sahara ambapo nchi hizo hutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano NICTBB.
Na:Amina Omar Zanzibar24
Post a Comment